Mwongozo huu umeandikwa kwa lengo la kumrahisishia mwanafunzi
au mwalimu kuchambua kazi yoyote ile ya fasihi. Mwandishi amelenga
na kuvijadili vipengele muhimu katika uchambuzi wa fasihi kama vile
uchambuzi wa jalada, anwani, ploti, dhamira, maudhui, mandhari,
wahusika na mbinu za kimtindo. Aidha, wanafunzi wamepewa shughuli
za kuwawezesha kukuza umilisi kama vile ushirikiano, uwazaji kina na
ujuzi wa kidijitali.